Saturday, April 28, 2012

MJUE DAKTARI BINGWA MSTAAFU ANAYEJISHUGHULISHA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MJINI BUKOBA.....

Daktari Bingwa Nusu Kafuti Modest Rwabubi,Daktari mstaafu ambaye amejikita katika kuboresha kilimo cha mbogamboga ili kuhifadhi mazingira.
Jamii ya wanaopenda mboga za majani upendelea kufika kwa Daktari huyu kujipatia mboga za majani zisizo na kemikali au chumvichumvi,Daktari mstaafu anapatikana maeneo ya uvukweni karibu na Kiroyera tours.
Mojawapo ya shughuli anazoshughulika nazo Daktari huyu ni kuhiofadhi mazingira,hapa anashiriki katika kupanda mti kama ishara ya kuhifadhi mazingira katika ofisi ya Bohari ya mkoa Kagera,huku akiwa na Meneja aliyeamishiwa mkoani Arusha Bw.Ntaita.

Wednesday, April 4, 2012

TUWAPENI MOYO WANAOJITOKEZA KUCHANGIA MAENDELEO YA ELIMU NCHINI

KEMONDO,BUKOBA VIJIJINI

IMEELEZWA kuwa jamii kutokubali kuchangia kwenye suala la ujenzi wa vyumba vya madara,ni changamoto kuu inayochangia kishusha maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Bukoba.

Hayo yalibainishwa na mkuu wa shule ya sekondari ya Kemondo Mwl.Charles Kalolora, iliyoko wilayani Bukoba mkoani Kagera,wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa vyumba vitano vya madarasa vilivyojengwa kwa nguvu ya ufadhiri kutoka wilayani humo.

Mwl.Karokola alisema kuwa jamii imekuwa ikisuasua katika michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,na kusababisha watumishi wa shule kufanya kazi katika mazingira magumu jambo ambalo linachangia kurudisha maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi.

Alisema maeneo mengi hali ya kukosa vyumba vya kufundishia ni kisababishi cha wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao,kwani kuwa na sehemu nzuri ya kufundishia ni sehemu inayochangia ufaulu wa wanafunzi katika mitihani yao ya mwaka.

Alisema kuwa shule hiyo pia,inakabiliwa na changamoto nyingine za muhimu kama vile kutokuwa na maabara kwa masomo ya sayansi,hali inayosababisha wanafunzi kushindwa kusoma kwa vitendo,kukosekana kwa maktaba pamoja na kutokuwa na walimu wa masomo ya hisabati na kiingereza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya shule Bi.Mary Karega,alitoa rai kwa wakazi wa mkoa wa Kagera kutambua na kudhamini mchango mkubwa uliotolewa na wafadhili mbali kwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa.

Bi.Karega ambaye ni mkurugenzi wa kiwanda cha Mapanki kilicho kata ya Kemondo,alitoa pongezi kwa wafadhili hao kwa mchango wao mkubwa wa kutambua hitaji la elimu kwa jamii,na kuwataka majirani wengine wanaopenda maendeleo kuiga mfano wa wanajamii hao waliojitokeza kitoa msaada wao huo.

Alisema jamii imekuwa na mtazamo wa kwamba mfadhili lazima iwe taasisi kubwa,kumbe hata mtu mmoja mmoja anaweza kujitolea kujenga chumba cha darasa ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwa jamii.

Aliwataja wafadhili walijitolea kufadhili ujenzi wa vyumba hivyo kuwa ni kampuni ya VicFish LTD iliyokamilisha ujenzi wa vyumba viwili,bw.Hamdan Suleiman,Kampuni ya Mapanki,bi.Saad Juma na Kemondo Ophans Care Center,ambao kila moja amejenga chumba kimoja kimoja kwa gharama ya shilingi 13.5 milioni kila chumba.

Katika taarifa ya meneja wa kampuni ya kusindika minofu ya samaki ya Vic Fish LTD iliyoko mjini Bukoba ilyosomwa kwa niaba yake na afisa utumishi wa kampuni Husein Buhuba,ujenzi wa vyumba hivyo umegharimu kiasi cha shilingi 23.5 milioni kupia mradi wa uvuvi endelevu,unaotekelezwa na kampuni hiyo.

Kwa upande wake meneja wa mradi wa uvuvi endelevu wa Vic Fish LTD,Jacob Maiseli,alisema msaada huo ni sehemu ya mradi kuangalia zaidi juu ya faida ya rasilimali za taifa inavyowasaidia wanajamii husika.Hivyo ni kujikita zaidi katika kurudisha fadhira kama sehemu ya kuendeleza jamii za wavuvi.

Maiseli alisema pamoja na kusaidia katika sekta ya elimu pia mradi huo unatekeleza katika mpango wa afya kwa kujenga vituo vya zahanati,kutoa huduma ya kiliniki kwa akina mama katika maeneo ya visiwani ambako ni Kerebe,Makibwa,Nyaburo,Nyabesige na Nyamukazi.

Alisema kuwa ufadhili wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kemondo umetokana na kuwepo na mwalo wa Rushara ambapo kiwanda cha Vic fish pia upokelea samaki kutoka kwa wavuvi hivyo ni jambo la muhimu kuchangia maendeleo ya eneo husika.

Monday, April 2, 2012

WALIMU WATARAJIWA EPUKENI USHAURI MWINGINE USIO NA TIJA JUU YA TAALUMA YENU..

BUKOBA-KAGERA

WANACHUO wa vyuo mbalimbali mkoani Kagera,wametakiwa kuepuka ushauri wenye nia yakuwapotosha kimalengo na baadala yake waelekeze kufuata mafundisho ya darasani ambayo kimsingi ndiyo mtazamo wao wa kimaisha.
Ushauri huo,umetolewa na mwalimu Rwekiti Michael ambaye pia ni mkuu wa chuo cha ualimu Nshabya kilichoko Manispaa ya Bukoba,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mwanachuo kufuata mafundisho ya darasani kwa kipindi chake cha masomo.
Rwekiti amebainisha kuwa kipindi cha kuwaandaa wanachuo kimasomo,kimaadili ya ualimu kunakuwepo changamoto nyingi,huku nyingi zikiwakabili wanachuo kwa nia ya kuwatoa katika malengo yao na kuwapotosha wakikose kile walichokusudia.
Mwalimu Rwekiti amesema kuwa wanakuwepo baadhi ya watu wanajitokeza kuwarubuni wanachuo kwa kuwapa ushauri ambao ni kinyume na malengo yao,hivyo wakati mwingine mwanachuo anaweza kukosa kile alicholenga kukipata juu ya taaluma yao.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa taaluma ya ualimu,chuo hicho kimejiwekea mpango wa kuandaa mwalimu bora na kwa maadili mema ili aweze kutoa mafundisho bora kwa vizazi vya waTanzania pale anapokuwa amehitimu mafunzo yake chuoni.
Hata hivy,mkuu huyo wa chuo,amesema kuwa uongozi wa chuo autasita adhabu au kuwachua hatua za kinidhamu kwa mwanachuo yeyote atakayebainika kukiuka itaratibu wa chuo hicho,kwani lengo kuu la chuo ni kumwandaa na kumpata mwalimu mwenye nidhamu na taalumu ili naye aweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi hapo baadaye.
Aidha,amewaasa wazazi na wadau mbalimbali mkoani hapa,kutoa ushirikiano kwa kuwapa maelekezo na ushauri mzuri wanachu hasa kipindi hiki wanapokaribia kufanya mitihani yao ya mwisho ili kuwapa moyo wakujituma na kutambua umuhimu wao katika jamii na umuhimu wa taaluma yao kitaifa.
Jumla ya wanachuo 78 wanatarajiwa kufanya mtihani wao wa mwisho huku wanachuo 93 wakiwa mwaka wa kwanza.
Chuo cha Ualimu cha Nshabya ni miongoni mwa vyuo vingine vitatu vya ualimu vilivyo ndani ya mkoa wa Kagera,na kimepata kusajiliwa tangu mwaka 2010,na kupatiwa namba ya usajili CU.108.

Friday, March 30, 2012

WAKULIMA KAGERA TUMIENI MBOLEA....

Ndizi ni zao kuu la chakula mkoani Kagera,wakulima wengi ustawisha zao ili bila kutumia mbolea,sasa wakati umefika zao hili nalo laanza kutoweka,changamoto kubwa yawaelekeza matumizi ya mbolea yaanze kupewa umuhimu.Picha kwa hisani ya www.bukobajamii.blogspot.

WAKULIMA ACHANA NA KULIMA BILA MBOLEA,SAMADI YA KUMWAGA YAOZA KAGOMA RANCHI

Bukoba Vijijini-KAGERA
WAKULIMA  mkoani Kagera wameshauliwa kutumia mbolea aina ya samadi inayopatikana kwa wingi katika sehemu za ranchi za Taifa(NARCO)ili kukabiliana na changamoto za udongo kukosa rutuba kwa baadhi ya maeneo mbalimbali ya kilimo cha mazao mbalimbali.

Akiongelea juu ya matumizi ya samadi, meneja wa ranchi ya Taifa(NARCO) ya Kagoma,Boniphasi Rwegila,alisema kuwa ni fursa pekee kwa wakazi wa mkoa wa Kagera kutumia ranchi zilizomo mkoani hapa kwa matumizi ya kilimo cha kisasa,jambo ambalo litawasaidia kupambana na umasikini wa kipato.

Rwegila alisema kuwa mbolea nyingi aina ya samadi iliyopo ndani ya ranchi ni mmojawapo ya fursa tosha wanayopata kunufaika nayo wananchi kwa kulipia gharama nafuu na kuchukua mbolea kwa madhumuni ya kulima na kuotesha mazao mengi.

Alisema kuwa ranchi(NARCO)imekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya manufaa yanaoweza kupatika kwa kutumia ranchi za taifa,ikiwemi kuhamasisha wananchi kufika maeneo ya ranchi na kuchukua mbolea kwa kulipia gharama kidogo,lengo ni kuwawezesha wananchi ili kunufaisha na rasilimali zao za Taifa.

Pia,alibainisha kuwa maeneo mengi mkoani Kagera yamekuwa yakitajwa kukosekana na rutuba na wakati mwingine huwa vigumu hata utumiaji wa mbolea za viwandani kwani pamoja na kuwa na gharama kubwa pia mila uchangia wananchi kutoshawishika kuzitumia mbolea hizo.Hivyo ni bora jamii ikahamasika kutumia mbolea(Samadi)inayopatikana kwa urahisi na inayokubarika kwa udongo wa mazingira husika.

Mbali na upatikanaji wa mbolea aina ya samadi kwa wingi,katika ranchi ya Taifa ya Kagoma iliyoko wilaya ya Bukoba vijijini na kupakana na wilaya za Muleba na Karagwe,pia ranchi hiyo inazalisha mbegu bora za ng'ombe ijulikanayo kwa jina 'Morani'ambazo usambazwa kwa wafugaji wadogo wadogo vijijini.

Rwegila alisema kuwa mpango wa kuzalisha mbegu bora aina ya Morani,umefanikiwa kwa kiasi kikubwa lengo la NARCO ni kuzalisha mbegu bora ya ng'ombe ambayo ina sifa ya kukua haraka,kuwa na nyama nzuri na kutoa maziwa mengi,hivyo ni muhimu kwa mkulima mdogo wa kijijini kwa kufuga mbegu inayo kua haraka na yenye soko kwa mahitaji ya sasa na kesho.

"Tumefanikiwa kwa kutoa mbegu bora za Morani na tumezisambaza kwa wakulima vijijini,ili waweze kubadirisha mbegu yao ya zamamani ijukana kwa jina la 'Nkole'ambayo uchelewa kukua na haitoi maziwa mengi kwa mfugaji"alisema Rwegila.

Hata hivyo,pamoja na malengo hayo juu ya kuinua pato la mkulima,pia zilitajwa baadhi za changamoto zinazokabili ranchi ya (NARCO)Kagoma,ikiwani mifugo kushambuliwa magonjwa ambayo yanadaiwa kutokana na baadhi ya mifugo kutoka kwa majirani wa ranchi na kusababisha shughuli za uendeshaji kuwa ngumu.

Alisema kuwa changamoto ya magonjwa ni chanjo ambapo madawa ni ghali mno na hii ni kutokana na serikali kujitoa kuhudumia ranchi za Taifa(NARCO)hivyo na kufanya ranchi zenyewe kujitegea katika shughuli za uendeshaji bila ruzuku ya uendeshaji kutoka serikali.

Kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO)inamiliki ranchi nne mkoani Kagera ambazo ni Kagoma iliyoko wilaya ya Bukoba vijijini,Missenyi na Mabale  zikiwa wilayani Missenyi huku Kikurula ikiwa wilayani Karagwe.

Tuesday, March 27, 2012

MHINDI AWAITA WAZAWA'NYANI' SASA HII KALI...

KEMONDO -BUKOBA.

WAFANYAKAZI wa kiwanda cha kusindika minofu ya samaki cha Kagera Fish Company ltd kilicho katika kata ya Kemondo wilayani Bukoba,wameulalamikia uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwafanyia vitendo vya uzalilishaji na kubambikiziwa kesi pale wanapodai haki zao za malipo.

Wafanyakazi hao(30) ambao majina yao yameifadhiwa kwa usalama wao,wamesema mwajili wao ambaye yamemtaja kwa jina moja la Awadesh ambaye ana asili ya kieshia kuwa amekuwa akiwatukana matusi ya uzalilishaji na kuwatishia kufunga iwapo wakiendelea kudai madai yao pale wanapokuwa wakidai haki zao kutokana na kazi wanazofanya kiwandani hapo.

Wameeleza kulazimishwa kufanya kazi nyingi kwa muda mwingi kuanzia asubuhi hadi asubuhi ya siku nyingine bila kupewa malipo ya ziada(over time)na wanapodai malipo yao,mwajili(Awadesh)umpigia simu mkuu wa kituo cha Polisi Kemondo(OCS)ambaye ufika mara moja na kuwakamata na kuwaweka maabusu.

Wamebainisha mhindi huyo(Awadesh)utumia muda mwingi kwa kuwatusi kwa kuwaita ‘nyani’jambo ambalo linawadharirisha na linaonyesha wazi kuwa hawadhaminiki kama binadamu mbele ya mwajili wao huyo japo kazi wanazozifanya ni nyingi na zinaingia uchumi taifa.

Aidha,wamesema kuwa mbali na kufanyakazi katika mazingira magumu,matusi yanazidi kila siku wawapo kazini huku wakimtaja Dayari Sin ambaye pia ni meneja uzalishaji(Production Manager) kiwandani hapo kuwa uwatusi na kuwakejeli kuwa hata waende kushitaki wapi hakuna watakaposikilizwa kwani hawana fedha.

“Ni muda mrefu tumedhurumiwa haki zetu,tukidai haki zetu tunakamatwa na polisi na kulazwa ndani,tunabambikiziwa kesi zisizo za kweli.huku wenzetu hawa(wahindi)wanatudharirisha na kusema wazi  kuwa Serikali yetu haina akiri,askari kuja chukua fedha kiwandani na kuondoka”walisema wahanga wa manyanyaso hayo.

Wamesema kuwa wanashangazwa kuona wahindi wanatumia kituo cha serikali yetu chenye dhamana ya kulinda usalama wetu,kutukandamiza na kudhurumu haki zetu kama vile kipo kwa ajili ya wamiliki wa kiwanda tu.

Alipotafutwa meneja mkuu wa Kiwanda hicho Awadesh hakutaka kuongelea juu ya jambo hilo mpaka alipomruhusu afisa utumishi wake Wilson John kuwa ndiye wakuongelea suala hilo.

Hata hivyo Wilson alikiri kuwepo hali hiyo ndani ya kiwanda hicho,na kudai kuwa yeye haoni sababu ya wafanyakazi kuendelea kuvurugana na mwajili wao,kama walikuja kufanya kazi ni bora wakubaliane na matakwa ya mwajili iwapo hawako tayari bora waache waende kwingine.

Alipoulizwa kuhusu kuwepo matunizi ya kituo cha polisi kwa maslahi ya kiwanda na nia ya kuwakandamiza wafanyakazi,alijibu kuwa hiyo hipo juu ya uwezo wake kwani ni mahusiano yaliopo baina ya mkuu wa kituo na kiwanda hicho.

Aidha,baadhi ya wakazi wa Kemondo wamelaani askari kutumiwa na kiwanda kuwakamata watendaji kwa kuwabambikizia kesi zisizo za kweli,kwani zipo nia za askari kufanya uchunguzi kabla ya kuingilia masuala ya watumishi hao.

Walisema kuwa mbali na madai hayo,kiwanda hicho pia kinakasoro kibao zikiwemo za kikwepa ushuru wa kulipia mabondo,kuwa na njama za kuyasafirisha usiku kwenda nchini Uganda.Na kuingiza samaki walio chini ya kiwango kinachokubalika(undersize)hasa wakati wa usiku wakidai serikali usiku uwa imelala.

Kiwanda cha kusindika minofu ya samaki cha Kagera Fish Company ltd,kina ubia na mwekezaji wa ndani Nadhir Karamagi kwa kushirikiana na menegimenti ya kiwanda kingine cha kusindika minofu cha Omega kilicho jijini Mwanza,kina jumla ya wafanyakazi wa kudumu 30 pamoja na vibarua zaidi ya 70.

Sunday, March 25, 2012

GHARAMA ZA UZALISHAJI ZINACHANGIA BEI YA SUKARI KUWA JUU

KYAKA-MISSENYI

UONGOZI wa kiwanda cha sukari cha Kagera(Kagera Sugar Limited)uesema kuwa bei ya sukario haipandishwi kiholela kwa maslahi ya kiwanda bali ni kutokana na kuwepo gharama kubwa za uzalishaji kiwandani.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi,mmoja wa watendaji wakuu katika kiwanda hicho,Vicent Mtaki,amekiri kuwa ni kweli bei ya sukari kwa wananchi wa mkoa wa Kagera ni ya juu kulinganisha na miaka ya nyuma lakini lazima na jamii itambue kuwa kiwanda kinatumia gharama kubwa hadi kufikia atua ya kuzalisha sukari.

Mtaki alisema kuwa kuwepo na gharama kubwa kunatokana na mkoa wa Kagera kuwa mbali sana na jiji la Dar es salaamu ambapo,mahitaji mengi juu ya shughuli za uzalishaji yanapatikana huko.

Alisema kuwa mkoa wa Kagera huko pembezoni mwa nchi,tofauti na mikoa mingine yenye viwanda vya kuzalisha sukari kama Morogoro ambapo ni rahisi kuchukua malighafi(raw materials)jijini Dar es salaamu tofauti na Kagera ambako ni vigumu kuzalisha sukari na kuiuza kwa bei ya chini huku kila mahitaji ya uzalishaji yanategemewa kupatikana Dar es salaam.

"Kuanzia chuma,mafuta ya Disel,pembejeo za kilimo,madawa nk vyote tunavinunua Dar es salaam,gharama inakuwa juu hasa kwa kipindi hiki cha mtikisiko wa uchumi duniani,hivyo tunalazimu kuzalisha kiwango ambacho tunakisambaza mikoa hasa ya Kagera na Mwanza ili kuepuka hasara kubwa kwani mbali na maeneo hayo kiwanda kitaingia hasara kubwa sana"alisema Mtaki.

Alisha kutokana na changamoto hiyo,inakuwa vigumu kiwanda kusambaza sukari kwa mikoa mingine tofauti na tajwa kwani iwapo kiwanda kitalazika kufanya hivyo,lazima bei ipande zaidi kwa wakazi wa mikoa mingine kutokana kuwepo na gharama za usafirishaji.

Hata hivyo,Mtaki amewatoa wasiwasi wananchi wa Kagera kuwa bei ya sukari kamwe haiwezi kuendelea kubaki pale ilipo,kwani watarajie kushuka iwapo hali ya mfumuko wa bei utakapo kuwa umepungua.

Kauli hiyo kwa uongozi wa kiwanda imekuja mara baada ya kuwepo minongono mingi kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kuhusu kutoshuka bei ya sukari ambapo hadi sasa kilo moja ya sukari inanunuliwa kati ya bei ya shilingi 2000/= hadi 2500/=jambo ambalo linawakatisha tamaa ya maisha wananchi huku wengi wakilinganisha iweje bei ya cement iuzwe 20000 kwa mfuko na ikiwa jijini Dar es Salaam iuzwe kati ya 13500 au 14000/=.