Saturday, April 28, 2012

MJUE DAKTARI BINGWA MSTAAFU ANAYEJISHUGHULISHA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MJINI BUKOBA.....

Daktari Bingwa Nusu Kafuti Modest Rwabubi,Daktari mstaafu ambaye amejikita katika kuboresha kilimo cha mbogamboga ili kuhifadhi mazingira.
Jamii ya wanaopenda mboga za majani upendelea kufika kwa Daktari huyu kujipatia mboga za majani zisizo na kemikali au chumvichumvi,Daktari mstaafu anapatikana maeneo ya uvukweni karibu na Kiroyera tours.
Mojawapo ya shughuli anazoshughulika nazo Daktari huyu ni kuhiofadhi mazingira,hapa anashiriki katika kupanda mti kama ishara ya kuhifadhi mazingira katika ofisi ya Bohari ya mkoa Kagera,huku akiwa na Meneja aliyeamishiwa mkoani Arusha Bw.Ntaita.

Wednesday, April 4, 2012

TUWAPENI MOYO WANAOJITOKEZA KUCHANGIA MAENDELEO YA ELIMU NCHINI

KEMONDO,BUKOBA VIJIJINI

IMEELEZWA kuwa jamii kutokubali kuchangia kwenye suala la ujenzi wa vyumba vya madara,ni changamoto kuu inayochangia kishusha maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Bukoba.

Hayo yalibainishwa na mkuu wa shule ya sekondari ya Kemondo Mwl.Charles Kalolora, iliyoko wilayani Bukoba mkoani Kagera,wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa vyumba vitano vya madarasa vilivyojengwa kwa nguvu ya ufadhiri kutoka wilayani humo.

Mwl.Karokola alisema kuwa jamii imekuwa ikisuasua katika michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,na kusababisha watumishi wa shule kufanya kazi katika mazingira magumu jambo ambalo linachangia kurudisha maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi.

Alisema maeneo mengi hali ya kukosa vyumba vya kufundishia ni kisababishi cha wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao,kwani kuwa na sehemu nzuri ya kufundishia ni sehemu inayochangia ufaulu wa wanafunzi katika mitihani yao ya mwaka.

Alisema kuwa shule hiyo pia,inakabiliwa na changamoto nyingine za muhimu kama vile kutokuwa na maabara kwa masomo ya sayansi,hali inayosababisha wanafunzi kushindwa kusoma kwa vitendo,kukosekana kwa maktaba pamoja na kutokuwa na walimu wa masomo ya hisabati na kiingereza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya shule Bi.Mary Karega,alitoa rai kwa wakazi wa mkoa wa Kagera kutambua na kudhamini mchango mkubwa uliotolewa na wafadhili mbali kwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa.

Bi.Karega ambaye ni mkurugenzi wa kiwanda cha Mapanki kilicho kata ya Kemondo,alitoa pongezi kwa wafadhili hao kwa mchango wao mkubwa wa kutambua hitaji la elimu kwa jamii,na kuwataka majirani wengine wanaopenda maendeleo kuiga mfano wa wanajamii hao waliojitokeza kitoa msaada wao huo.

Alisema jamii imekuwa na mtazamo wa kwamba mfadhili lazima iwe taasisi kubwa,kumbe hata mtu mmoja mmoja anaweza kujitolea kujenga chumba cha darasa ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwa jamii.

Aliwataja wafadhili walijitolea kufadhili ujenzi wa vyumba hivyo kuwa ni kampuni ya VicFish LTD iliyokamilisha ujenzi wa vyumba viwili,bw.Hamdan Suleiman,Kampuni ya Mapanki,bi.Saad Juma na Kemondo Ophans Care Center,ambao kila moja amejenga chumba kimoja kimoja kwa gharama ya shilingi 13.5 milioni kila chumba.

Katika taarifa ya meneja wa kampuni ya kusindika minofu ya samaki ya Vic Fish LTD iliyoko mjini Bukoba ilyosomwa kwa niaba yake na afisa utumishi wa kampuni Husein Buhuba,ujenzi wa vyumba hivyo umegharimu kiasi cha shilingi 23.5 milioni kupia mradi wa uvuvi endelevu,unaotekelezwa na kampuni hiyo.

Kwa upande wake meneja wa mradi wa uvuvi endelevu wa Vic Fish LTD,Jacob Maiseli,alisema msaada huo ni sehemu ya mradi kuangalia zaidi juu ya faida ya rasilimali za taifa inavyowasaidia wanajamii husika.Hivyo ni kujikita zaidi katika kurudisha fadhira kama sehemu ya kuendeleza jamii za wavuvi.

Maiseli alisema pamoja na kusaidia katika sekta ya elimu pia mradi huo unatekeleza katika mpango wa afya kwa kujenga vituo vya zahanati,kutoa huduma ya kiliniki kwa akina mama katika maeneo ya visiwani ambako ni Kerebe,Makibwa,Nyaburo,Nyabesige na Nyamukazi.

Alisema kuwa ufadhili wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kemondo umetokana na kuwepo na mwalo wa Rushara ambapo kiwanda cha Vic fish pia upokelea samaki kutoka kwa wavuvi hivyo ni jambo la muhimu kuchangia maendeleo ya eneo husika.

Monday, April 2, 2012

WALIMU WATARAJIWA EPUKENI USHAURI MWINGINE USIO NA TIJA JUU YA TAALUMA YENU..

BUKOBA-KAGERA

WANACHUO wa vyuo mbalimbali mkoani Kagera,wametakiwa kuepuka ushauri wenye nia yakuwapotosha kimalengo na baadala yake waelekeze kufuata mafundisho ya darasani ambayo kimsingi ndiyo mtazamo wao wa kimaisha.
Ushauri huo,umetolewa na mwalimu Rwekiti Michael ambaye pia ni mkuu wa chuo cha ualimu Nshabya kilichoko Manispaa ya Bukoba,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mwanachuo kufuata mafundisho ya darasani kwa kipindi chake cha masomo.
Rwekiti amebainisha kuwa kipindi cha kuwaandaa wanachuo kimasomo,kimaadili ya ualimu kunakuwepo changamoto nyingi,huku nyingi zikiwakabili wanachuo kwa nia ya kuwatoa katika malengo yao na kuwapotosha wakikose kile walichokusudia.
Mwalimu Rwekiti amesema kuwa wanakuwepo baadhi ya watu wanajitokeza kuwarubuni wanachuo kwa kuwapa ushauri ambao ni kinyume na malengo yao,hivyo wakati mwingine mwanachuo anaweza kukosa kile alicholenga kukipata juu ya taaluma yao.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa taaluma ya ualimu,chuo hicho kimejiwekea mpango wa kuandaa mwalimu bora na kwa maadili mema ili aweze kutoa mafundisho bora kwa vizazi vya waTanzania pale anapokuwa amehitimu mafunzo yake chuoni.
Hata hivy,mkuu huyo wa chuo,amesema kuwa uongozi wa chuo autasita adhabu au kuwachua hatua za kinidhamu kwa mwanachuo yeyote atakayebainika kukiuka itaratibu wa chuo hicho,kwani lengo kuu la chuo ni kumwandaa na kumpata mwalimu mwenye nidhamu na taalumu ili naye aweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi hapo baadaye.
Aidha,amewaasa wazazi na wadau mbalimbali mkoani hapa,kutoa ushirikiano kwa kuwapa maelekezo na ushauri mzuri wanachu hasa kipindi hiki wanapokaribia kufanya mitihani yao ya mwisho ili kuwapa moyo wakujituma na kutambua umuhimu wao katika jamii na umuhimu wa taaluma yao kitaifa.
Jumla ya wanachuo 78 wanatarajiwa kufanya mtihani wao wa mwisho huku wanachuo 93 wakiwa mwaka wa kwanza.
Chuo cha Ualimu cha Nshabya ni miongoni mwa vyuo vingine vitatu vya ualimu vilivyo ndani ya mkoa wa Kagera,na kimepata kusajiliwa tangu mwaka 2010,na kupatiwa namba ya usajili CU.108.