WANACHUO
wa vyuo mbalimbali mkoani Kagera,wametakiwa kuepuka ushauri wenye nia
yakuwapotosha kimalengo na baadala yake waelekeze kufuata mafundisho ya
darasani ambayo kimsingi ndiyo mtazamo wao wa kimaisha.
Ushauri
huo,umetolewa na mwalimu Rwekiti Michael ambaye pia ni mkuu wa chuo cha
ualimu Nshabya kilichoko Manispaa ya Bukoba,wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mwanachuo kufuata mafundisho ya
darasani kwa kipindi chake cha masomo.
Rwekiti
amebainisha kuwa kipindi cha kuwaandaa wanachuo kimasomo,kimaadili ya
ualimu kunakuwepo changamoto nyingi,huku nyingi zikiwakabili wanachuo
kwa nia ya kuwatoa katika malengo yao na kuwapotosha wakikose kile
walichokusudia.
Mwalimu Rwekiti amesema
kuwa wanakuwepo baadhi ya watu wanajitokeza kuwarubuni wanachuo kwa
kuwapa ushauri ambao ni kinyume na malengo yao,hivyo wakati mwingine
mwanachuo anaweza kukosa kile alicholenga kukipata juu ya taaluma yao.
Amesema
kwa kutambua umuhimu wa taaluma ya ualimu,chuo hicho kimejiwekea mpango
wa kuandaa mwalimu bora na kwa maadili mema ili aweze kutoa mafundisho
bora kwa vizazi vya waTanzania pale anapokuwa amehitimu mafunzo yake
chuoni.
Hata
hivy,mkuu huyo wa chuo,amesema kuwa uongozi wa chuo autasita adhabu au
kuwachua hatua za kinidhamu kwa mwanachuo yeyote atakayebainika kukiuka
itaratibu wa chuo hicho,kwani lengo kuu la chuo ni kumwandaa na kumpata
mwalimu mwenye nidhamu na taalumu ili
naye aweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi hapo baadaye.
Aidha,amewaasa
wazazi na wadau mbalimbali mkoani hapa,kutoa ushirikiano kwa kuwapa
maelekezo na ushauri mzuri wanachu hasa kipindi hiki wanapokaribia
kufanya mitihani yao ya mwisho ili kuwapa moyo wakujituma na kutambua
umuhimu wao katika jamii na umuhimu wa taaluma yao kitaifa.
Jumla ya wanachuo 78 wanatarajiwa kufanya mtihani wao wa mwisho huku wanachuo 93 wakiwa mwaka wa kwanza.
Chuo
cha Ualimu cha Nshabya ni miongoni mwa vyuo vingine vitatu vya ualimu
vilivyo ndani ya mkoa wa Kagera,na kimepata kusajiliwa tangu mwaka 2010,na
kupatiwa namba ya usajili CU.108.
No comments:
Post a Comment