KEMONDO,BUKOBA VIJIJINI
IMEELEZWA kuwa jamii
kutokubali kuchangia kwenye suala la ujenzi wa vyumba vya madara,ni
changamoto kuu inayochangia kishusha maendeleo ya kitaaluma kwa
wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Bukoba.
Hayo
yalibainishwa na mkuu wa shule ya sekondari ya Kemondo Mwl.Charles
Kalolora, iliyoko wilayani Bukoba mkoani Kagera,wakati wa hafla fupi ya
kukabidhiwa vyumba vitano vya madarasa vilivyojengwa kwa nguvu ya
ufadhiri kutoka wilayani humo.
Mwl.Karokola alisema kuwa jamii
imekuwa ikisuasua katika michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,na
kusababisha watumishi wa shule kufanya kazi katika mazingira magumu
jambo ambalo linachangia kurudisha maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi.
Alisema maeneo mengi hali ya kukosa vyumba vya kufundishia ni kisababishi cha wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika
mitihani yao,kwani kuwa na sehemu nzuri ya kufundishia ni sehemu inayochangia ufaulu wa wanafunzi katika mitihani yao ya mwaka.
Alisema
kuwa shule hiyo pia,inakabiliwa na changamoto nyingine za muhimu kama
vile kutokuwa na maabara kwa masomo ya sayansi,hali inayosababisha
wanafunzi kushindwa kusoma kwa vitendo,kukosekana kwa maktaba pamoja na
kutokuwa na walimu wa masomo ya hisabati na kiingereza.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa bodi ya shule Bi.Mary Karega,alitoa rai kwa
wakazi wa mkoa wa Kagera kutambua na kudhamini mchango mkubwa uliotolewa
na wafadhili mbali kwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vitano vya
madarasa.
Bi.Karega ambaye ni mkurugenzi wa kiwanda cha Mapanki
kilicho kata ya Kemondo,alitoa pongezi kwa wafadhili hao kwa mchango wao
mkubwa wa kutambua hitaji la elimu kwa jamii,na kuwataka majirani
wengine wanaopenda maendeleo kuiga mfano wa wanajamii hao waliojitokeza
kitoa msaada wao huo.
Alisema jamii imekuwa na
mtazamo wa kwamba mfadhili lazima iwe taasisi kubwa,kumbe hata mtu
mmoja mmoja anaweza kujitolea kujenga chumba cha darasa ikiwa ni sehemu
ya mchango wake kwa jamii.
Aliwataja wafadhili walijitolea
kufadhili ujenzi wa vyumba hivyo kuwa ni kampuni ya VicFish LTD
iliyokamilisha ujenzi wa vyumba viwili,bw.Hamdan Suleiman,Kampuni ya
Mapanki,bi.Saad Juma na Kemondo Ophans Care Center,ambao kila moja
amejenga chumba kimoja kimoja kwa gharama ya shilingi 13.5 milioni kila
chumba.
Katika taarifa ya meneja wa kampuni ya kusindika minofu
ya samaki ya Vic Fish LTD iliyoko mjini Bukoba ilyosomwa kwa niaba yake
na afisa utumishi wa kampuni Husein Buhuba,ujenzi wa vyumba hivyo
umegharimu kiasi cha shilingi 23.5 milioni kupia mradi wa uvuvi
endelevu,unaotekelezwa na kampuni hiyo.
Kwa upande wake meneja wa
mradi wa uvuvi endelevu wa Vic Fish LTD,Jacob Maiseli,alisema msaada
huo ni sehemu ya mradi kuangalia zaidi juu ya faida ya rasilimali za
taifa
inavyowasaidia wanajamii husika.Hivyo ni kujikita zaidi katika
kurudisha fadhira kama sehemu ya kuendeleza jamii za wavuvi.
Maiseli
alisema pamoja na kusaidia katika sekta ya elimu pia mradi huo
unatekeleza katika mpango wa afya kwa kujenga vituo vya zahanati,kutoa
huduma ya kiliniki kwa akina mama katika maeneo ya visiwani ambako ni
Kerebe,Makibwa,Nyaburo,Nyabesige na Nyamukazi.
Alisema kuwa
ufadhili wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari ya
Kemondo umetokana na kuwepo na mwalo wa Rushara ambapo kiwanda cha Vic
fish pia upokelea samaki kutoka kwa wavuvi hivyo ni jambo la muhimu
kuchangia maendeleo ya eneo husika.
No comments:
Post a Comment