CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)kimeendeleza kampeini yake ya kuhamasisha wananchi kukiunga mkono katika jimbo la Muleba kusini,na kufanikiwa kupata jumla ya wanachama wapya 112 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa red cross mjini Muleba jana jioni.
Shamrashamra hizo za CHADEMA zilitanguliwa na ufunguzi wa ofisi ya chama ya jimbo la Muleba kusini lililoko wilayani Muleba,jimbo ambali kwa sasa linashikiliwa na mbunge wa CCM ambaye pia ni waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka.
Mkutano huo uliokuwa umemkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kagera Wilfred Rwakatare,ulihudhuriwa na wananchi wengi kutoka sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kagera pamoja na kuhudhuriwa na mbunge wa viti maalumu Chadema Conchesta Rwamulaza,Anna Mukono ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chadema mkoani hapa pamoja na madiwani mbalimbali kutoka vyamma vingine vya upinzani vilivyo ndani ya wilaya ya Muleba.
Katika mkutano huo,chama hicho kiliweza kuvuna idadi ya wanachama wapya ndani ya chama hicho 112,huku wanachama 45 walirudisha kadi kutoka vyama vingine vya siasa na wanachama 67 walijiunga kwa kununua kadi na kujisajili upya.
Baadhi ya wanachama walioweza kujiunga chama hicho kwa kurudisha kadi ni 21 kutoka CCM,wanachama 11 kutoka TLP,wanachama 7 kutoka CUF na wanachama 6 kutoka NCCR Mageuzi.
Aidha,chama hicho kiliendesha harambee ili kupata mchango wa kuweza kuendesha ofisi jimboni hapo,ambapo harambee hiyo iliendeshwa na diwani wa kata ya Buseresere wilayani Chato mkoani Geita Sprian Kagoma na kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 485,000/=ikiwa ni fedha taslimu.
No comments:
Post a Comment