Friday, March 30, 2012

WAKULIMA KAGERA TUMIENI MBOLEA....

Ndizi ni zao kuu la chakula mkoani Kagera,wakulima wengi ustawisha zao ili bila kutumia mbolea,sasa wakati umefika zao hili nalo laanza kutoweka,changamoto kubwa yawaelekeza matumizi ya mbolea yaanze kupewa umuhimu.Picha kwa hisani ya www.bukobajamii.blogspot.

WAKULIMA ACHANA NA KULIMA BILA MBOLEA,SAMADI YA KUMWAGA YAOZA KAGOMA RANCHI

Bukoba Vijijini-KAGERA
WAKULIMA  mkoani Kagera wameshauliwa kutumia mbolea aina ya samadi inayopatikana kwa wingi katika sehemu za ranchi za Taifa(NARCO)ili kukabiliana na changamoto za udongo kukosa rutuba kwa baadhi ya maeneo mbalimbali ya kilimo cha mazao mbalimbali.

Akiongelea juu ya matumizi ya samadi, meneja wa ranchi ya Taifa(NARCO) ya Kagoma,Boniphasi Rwegila,alisema kuwa ni fursa pekee kwa wakazi wa mkoa wa Kagera kutumia ranchi zilizomo mkoani hapa kwa matumizi ya kilimo cha kisasa,jambo ambalo litawasaidia kupambana na umasikini wa kipato.

Rwegila alisema kuwa mbolea nyingi aina ya samadi iliyopo ndani ya ranchi ni mmojawapo ya fursa tosha wanayopata kunufaika nayo wananchi kwa kulipia gharama nafuu na kuchukua mbolea kwa madhumuni ya kulima na kuotesha mazao mengi.

Alisema kuwa ranchi(NARCO)imekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya manufaa yanaoweza kupatika kwa kutumia ranchi za taifa,ikiwemi kuhamasisha wananchi kufika maeneo ya ranchi na kuchukua mbolea kwa kulipia gharama kidogo,lengo ni kuwawezesha wananchi ili kunufaisha na rasilimali zao za Taifa.

Pia,alibainisha kuwa maeneo mengi mkoani Kagera yamekuwa yakitajwa kukosekana na rutuba na wakati mwingine huwa vigumu hata utumiaji wa mbolea za viwandani kwani pamoja na kuwa na gharama kubwa pia mila uchangia wananchi kutoshawishika kuzitumia mbolea hizo.Hivyo ni bora jamii ikahamasika kutumia mbolea(Samadi)inayopatikana kwa urahisi na inayokubarika kwa udongo wa mazingira husika.

Mbali na upatikanaji wa mbolea aina ya samadi kwa wingi,katika ranchi ya Taifa ya Kagoma iliyoko wilaya ya Bukoba vijijini na kupakana na wilaya za Muleba na Karagwe,pia ranchi hiyo inazalisha mbegu bora za ng'ombe ijulikanayo kwa jina 'Morani'ambazo usambazwa kwa wafugaji wadogo wadogo vijijini.

Rwegila alisema kuwa mpango wa kuzalisha mbegu bora aina ya Morani,umefanikiwa kwa kiasi kikubwa lengo la NARCO ni kuzalisha mbegu bora ya ng'ombe ambayo ina sifa ya kukua haraka,kuwa na nyama nzuri na kutoa maziwa mengi,hivyo ni muhimu kwa mkulima mdogo wa kijijini kwa kufuga mbegu inayo kua haraka na yenye soko kwa mahitaji ya sasa na kesho.

"Tumefanikiwa kwa kutoa mbegu bora za Morani na tumezisambaza kwa wakulima vijijini,ili waweze kubadirisha mbegu yao ya zamamani ijukana kwa jina la 'Nkole'ambayo uchelewa kukua na haitoi maziwa mengi kwa mfugaji"alisema Rwegila.

Hata hivyo,pamoja na malengo hayo juu ya kuinua pato la mkulima,pia zilitajwa baadhi za changamoto zinazokabili ranchi ya (NARCO)Kagoma,ikiwani mifugo kushambuliwa magonjwa ambayo yanadaiwa kutokana na baadhi ya mifugo kutoka kwa majirani wa ranchi na kusababisha shughuli za uendeshaji kuwa ngumu.

Alisema kuwa changamoto ya magonjwa ni chanjo ambapo madawa ni ghali mno na hii ni kutokana na serikali kujitoa kuhudumia ranchi za Taifa(NARCO)hivyo na kufanya ranchi zenyewe kujitegea katika shughuli za uendeshaji bila ruzuku ya uendeshaji kutoka serikali.

Kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO)inamiliki ranchi nne mkoani Kagera ambazo ni Kagoma iliyoko wilaya ya Bukoba vijijini,Missenyi na Mabale  zikiwa wilayani Missenyi huku Kikurula ikiwa wilayani Karagwe.

Tuesday, March 27, 2012

MHINDI AWAITA WAZAWA'NYANI' SASA HII KALI...

KEMONDO -BUKOBA.

WAFANYAKAZI wa kiwanda cha kusindika minofu ya samaki cha Kagera Fish Company ltd kilicho katika kata ya Kemondo wilayani Bukoba,wameulalamikia uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwafanyia vitendo vya uzalilishaji na kubambikiziwa kesi pale wanapodai haki zao za malipo.

Wafanyakazi hao(30) ambao majina yao yameifadhiwa kwa usalama wao,wamesema mwajili wao ambaye yamemtaja kwa jina moja la Awadesh ambaye ana asili ya kieshia kuwa amekuwa akiwatukana matusi ya uzalilishaji na kuwatishia kufunga iwapo wakiendelea kudai madai yao pale wanapokuwa wakidai haki zao kutokana na kazi wanazofanya kiwandani hapo.

Wameeleza kulazimishwa kufanya kazi nyingi kwa muda mwingi kuanzia asubuhi hadi asubuhi ya siku nyingine bila kupewa malipo ya ziada(over time)na wanapodai malipo yao,mwajili(Awadesh)umpigia simu mkuu wa kituo cha Polisi Kemondo(OCS)ambaye ufika mara moja na kuwakamata na kuwaweka maabusu.

Wamebainisha mhindi huyo(Awadesh)utumia muda mwingi kwa kuwatusi kwa kuwaita ‘nyani’jambo ambalo linawadharirisha na linaonyesha wazi kuwa hawadhaminiki kama binadamu mbele ya mwajili wao huyo japo kazi wanazozifanya ni nyingi na zinaingia uchumi taifa.

Aidha,wamesema kuwa mbali na kufanyakazi katika mazingira magumu,matusi yanazidi kila siku wawapo kazini huku wakimtaja Dayari Sin ambaye pia ni meneja uzalishaji(Production Manager) kiwandani hapo kuwa uwatusi na kuwakejeli kuwa hata waende kushitaki wapi hakuna watakaposikilizwa kwani hawana fedha.

“Ni muda mrefu tumedhurumiwa haki zetu,tukidai haki zetu tunakamatwa na polisi na kulazwa ndani,tunabambikiziwa kesi zisizo za kweli.huku wenzetu hawa(wahindi)wanatudharirisha na kusema wazi  kuwa Serikali yetu haina akiri,askari kuja chukua fedha kiwandani na kuondoka”walisema wahanga wa manyanyaso hayo.

Wamesema kuwa wanashangazwa kuona wahindi wanatumia kituo cha serikali yetu chenye dhamana ya kulinda usalama wetu,kutukandamiza na kudhurumu haki zetu kama vile kipo kwa ajili ya wamiliki wa kiwanda tu.

Alipotafutwa meneja mkuu wa Kiwanda hicho Awadesh hakutaka kuongelea juu ya jambo hilo mpaka alipomruhusu afisa utumishi wake Wilson John kuwa ndiye wakuongelea suala hilo.

Hata hivyo Wilson alikiri kuwepo hali hiyo ndani ya kiwanda hicho,na kudai kuwa yeye haoni sababu ya wafanyakazi kuendelea kuvurugana na mwajili wao,kama walikuja kufanya kazi ni bora wakubaliane na matakwa ya mwajili iwapo hawako tayari bora waache waende kwingine.

Alipoulizwa kuhusu kuwepo matunizi ya kituo cha polisi kwa maslahi ya kiwanda na nia ya kuwakandamiza wafanyakazi,alijibu kuwa hiyo hipo juu ya uwezo wake kwani ni mahusiano yaliopo baina ya mkuu wa kituo na kiwanda hicho.

Aidha,baadhi ya wakazi wa Kemondo wamelaani askari kutumiwa na kiwanda kuwakamata watendaji kwa kuwabambikizia kesi zisizo za kweli,kwani zipo nia za askari kufanya uchunguzi kabla ya kuingilia masuala ya watumishi hao.

Walisema kuwa mbali na madai hayo,kiwanda hicho pia kinakasoro kibao zikiwemo za kikwepa ushuru wa kulipia mabondo,kuwa na njama za kuyasafirisha usiku kwenda nchini Uganda.Na kuingiza samaki walio chini ya kiwango kinachokubalika(undersize)hasa wakati wa usiku wakidai serikali usiku uwa imelala.

Kiwanda cha kusindika minofu ya samaki cha Kagera Fish Company ltd,kina ubia na mwekezaji wa ndani Nadhir Karamagi kwa kushirikiana na menegimenti ya kiwanda kingine cha kusindika minofu cha Omega kilicho jijini Mwanza,kina jumla ya wafanyakazi wa kudumu 30 pamoja na vibarua zaidi ya 70.

Sunday, March 25, 2012

GHARAMA ZA UZALISHAJI ZINACHANGIA BEI YA SUKARI KUWA JUU

KYAKA-MISSENYI

UONGOZI wa kiwanda cha sukari cha Kagera(Kagera Sugar Limited)uesema kuwa bei ya sukario haipandishwi kiholela kwa maslahi ya kiwanda bali ni kutokana na kuwepo gharama kubwa za uzalishaji kiwandani.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi,mmoja wa watendaji wakuu katika kiwanda hicho,Vicent Mtaki,amekiri kuwa ni kweli bei ya sukari kwa wananchi wa mkoa wa Kagera ni ya juu kulinganisha na miaka ya nyuma lakini lazima na jamii itambue kuwa kiwanda kinatumia gharama kubwa hadi kufikia atua ya kuzalisha sukari.

Mtaki alisema kuwa kuwepo na gharama kubwa kunatokana na mkoa wa Kagera kuwa mbali sana na jiji la Dar es salaamu ambapo,mahitaji mengi juu ya shughuli za uzalishaji yanapatikana huko.

Alisema kuwa mkoa wa Kagera huko pembezoni mwa nchi,tofauti na mikoa mingine yenye viwanda vya kuzalisha sukari kama Morogoro ambapo ni rahisi kuchukua malighafi(raw materials)jijini Dar es salaamu tofauti na Kagera ambako ni vigumu kuzalisha sukari na kuiuza kwa bei ya chini huku kila mahitaji ya uzalishaji yanategemewa kupatikana Dar es salaam.

"Kuanzia chuma,mafuta ya Disel,pembejeo za kilimo,madawa nk vyote tunavinunua Dar es salaam,gharama inakuwa juu hasa kwa kipindi hiki cha mtikisiko wa uchumi duniani,hivyo tunalazimu kuzalisha kiwango ambacho tunakisambaza mikoa hasa ya Kagera na Mwanza ili kuepuka hasara kubwa kwani mbali na maeneo hayo kiwanda kitaingia hasara kubwa sana"alisema Mtaki.

Alisha kutokana na changamoto hiyo,inakuwa vigumu kiwanda kusambaza sukari kwa mikoa mingine tofauti na tajwa kwani iwapo kiwanda kitalazika kufanya hivyo,lazima bei ipande zaidi kwa wakazi wa mikoa mingine kutokana kuwepo na gharama za usafirishaji.

Hata hivyo,Mtaki amewatoa wasiwasi wananchi wa Kagera kuwa bei ya sukari kamwe haiwezi kuendelea kubaki pale ilipo,kwani watarajie kushuka iwapo hali ya mfumuko wa bei utakapo kuwa umepungua.

Kauli hiyo kwa uongozi wa kiwanda imekuja mara baada ya kuwepo minongono mingi kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kuhusu kutoshuka bei ya sukari ambapo hadi sasa kilo moja ya sukari inanunuliwa kati ya bei ya shilingi 2000/= hadi 2500/=jambo ambalo linawakatisha tamaa ya maisha wananchi huku wengi wakilinganisha iweje bei ya cement iuzwe 20000 kwa mfuko na ikiwa jijini Dar es Salaam iuzwe kati ya 13500 au 14000/=.


Saturday, March 24, 2012

JESHI LA POLISI LAKIRI ASKARI WAKE KUAWA MGODINI





IGP Saidi Mwema,mmojawapo ya sehemu alipokuwa akitoa maelekezo ya kupambana na uharifu kwa jeshi la Polisi,Picha kwa hisani ya mjengwablog

JESHI LA POLISI LAKIRI ASKARI WAKE KUAWA

WATU wasiojulikana wanasakwa na jeshi la Polisi mkoani Kagera,kwa kuhusika na mauaji ya askari aliyekuwa lindo katika mgodi wa madini wa Tulawaka ulioko wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
 
Tukio la mauaji askari huyo PC.Dikson(29)G.2626,lilitokea jana majira ya saa 11 jioni,ambako marehemu alikutwa tayari ameuawa kwa kuchomwa na chuma(moko)kichwani,jambo ambalo liliwashangaza askari wenzake walikokuwa nae lindo.
 
Kwa mjibu wa kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Hennry Salewi,mwili wa marehemu uligunduliwa na wenzake mara baada ya kuwa na wasiwasi na mwenzake kwani ilikuwa ni dakika 15 tu marehemu alizunguka ukuta wa mgodi kama kawaida ya askari ndipo mauti yalipo mkuta.
 
Salewi alisema kuwa yawezekana muuaji alikuwa amemtegeshea askari huyo kwa nia ya kumuua na kutokomea na bunduki jambo ambalo muuaji alifanikiwa kwani aliweza kumvizia askari na kumugonga na Moko bila marehemu kupiga kelele,jambo linalosikitisha sana.
 
Alisema mbali na mauji hayo,pia wauaji walitokomea na bunduki aina ya SMG iliyokuwa na risasi 46,ambavyo mpaka sasa jeshi la polisi linaendelea na msako mkari wa majambazi hao katika mapori yaliyoko wilayani Biharamulo,huku akitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pale watakapo washuku wahusika ili kuweza kuwakamata mara moja.
 
Marehemu ameacha mke mjamzito na tayari mwili wake umeanza safari ya kuelekea nyumbani kwao Sumbawanga mkoani Rukwa.
 
Wakati huo huo,mwanamke mmoja Hadija Nassoro(19)mkazi wa kitongoji Kaishakila kijiji Kazinga kata Kaibanja wilayani Bukoba vijijini anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kusababisha mauaji ya mwanae.
 
Mtuhumiwa anatuhumiwa kwa kumtupa kwenye shimo la takataka mtoto mchanga Amir Haji(mwenye umri wa wiki mbili na siku mbili)na mwili wa marehemu uligunduliwa na wasamalia wema ndipo walipotoa taarifa na mtuhumiwa kukamatwa na tayari atua za kumpeleka mahakamani zimekamilika ili kusomewa shitaka linalomkasbiri.
 

Thursday, March 22, 2012

WIKI YA MAJI BILA MAJI............

Kwa miaka mingi serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha wananchi tunapata maji safi na salama. Maadhimisho ya wiki ya maji ni mojawapo ya jitihada, ambapo kwangu mimi naona inalenga kutoa elimu na fursa kwa wadau mbalimbali weweze kujadili namna ya kuboresha huduma hii hasa kwa maeneo ya vijijini ambapo imendeelea kuwa ndoto. Swali ni kuwa, kwetu sisi wananchi maadhimisho ya maji yanapaswa kutusaidia nini?
Nauliza swali hili kwa kuwa tumeshuhudia mengi yakifanywa kwa lengo la kuboresha huduma ya maji lakini bado matokeo ya juhudi hizi hayajatufikia sisi wananchi.
Wiki iliyokwisha, Umoja wa Mataifa ulizindua ripoti ya kimataifa ya hali ya upatikanaji huduma ya maji. Ripoti hiyo inaonesha kuwa kimataifa malengo ya milenia kuhusu maji yamefikiwa, ambapo asilimia 89% ya watu duniani wanapata maji kupitia vituo vya maji (vichoteo vya maji) vilivyoboreshwa.
Wakati dunia ikifurahia hatua hii nzuri, hali ni tofauti hapa kwetu Tanzania. Ripoti inaonesha kuwa hali ya huduma ya maji imekuwa ikidhorota na hata kupungua badala ya kuwa bora. Ripoti hiyo inaonesha kuwa asilimia 53% (mwaka 2010) ya watu hapa Tanzania wanapata huduma ya maji kutoka vituo vilivyoboreshwa. Huduma hii imepungua kwa asilimia 2% ambapo mwaka 1990 watu asilimia 55% walikuwa wanapata huduma ya maji.
Kwa mlinganisho, ripoti inaonesha kuwa ni nchi kumi na moja tuu zenye hali mbaya ya upatikanaji maji duniani kuliko Tanzania. Picha hii inazidi kuwa mbaya tunapolinganisha hali yetu ya huduma ya maji na nchi tisa za Afrika Mashariki.
 Mwaka 1990, tulikuwa nyuma ya nchi mbili tu Burudi na Rwanda kwenye upatikanaji wa maji safi na salama. Lakini kwa ripoti hii ya mwaka 2010, Malawi, Uganda, Zambia na Kenya zimetupita kwenye utoaji wa huduma ya maji. Sasa ni Msumbiji na Ethiopia tu ndio zipo nyuma yetu kwa utoaji wa huduma za Maji.
Ikumbukwe kuwa, katika kipindi cha miaka 20, 1990 hadi 2010, serikali imechukua jitihada mbali mbali ili kuboresha huduma ya maji nchini. Jitihada hizo ni pamoja kuanzisha sera ya maji, ambapo sera hii ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002 na kufanya maji kuwa bidhaa na sio huduma.
Sera hii ililenga kuwashirikisha wananchi katika kusimamia na kuendesha miradi ya maji. Pia serikali imekuwa ikiongeza bajeti ya maji mfano bajeti ya maendeleo ya maji vijijini iliongezeka kutoka 19bilioni mwaka 2005/06 hadi 124 bilioni mwaka 2009/2010.
 Sambamba na ongezeko la bajeti, Programu ya Mendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP). Program hii imekuwa na awamu mbili ambapo awamu ya kwanza kulikuwa na miradi ya matokeo ya haraka (Quick Win Projects) na awamu ya pili miradi ya vijiji kumi kila wilaya maarufu kama miradi ya benki ya dunia.

Jitihada hizi zimehusisha rasilimali nyingi sana za ndani na nyingine ni misaada na mikopo. Lakini bado matokeo ya jumla katika kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji Tanzania yamezidi kuwa hafuifu kama ambavyo ripoti hii inavyoonesha. Je, tunakosea wapi? tuendelee kuwekeza kwenye hii sekta isiyokuwa na matokea chanya?
Kwa hali hii gari linakuwa linarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Wizara ya maji, na wadau wote wa maji tufanye nini kuboresha hali hii? Je tunafahamu kiini cha tatizo? Kwa mtazamo wangu mojawapo ya tatizo ni kutodumu kwa miradi ya maji.
Tumekuwa tukiwekeza kila mwaka kujenga miradi mipya ya maji, lakini juhudi zetu zimekuwa zikienda sambamba na kufa kwa miundombinu ya maji.
Sensa ya utambuzi wa vituo vya maji iliyofanywa na GEODATA na WaterAid mwaka 2005 hadi 2009 kwenye wilaya 48 inaonesha kuwa asilimia 44% ya vituo vya maji vilivyoboreshwa havifanyi kazi. Sensa hiyo pia inaonesha kuwa, kila baada ya miaka miwili asilimia 25 ya miradi ya maji inakuwa tayari imeshakufa. Je ni kwanini miradi ya maji haidumu?
Imefika wakati sasa tuache kuwekeza katika kujenga miradi mipya ya maji, badala yake tuongeze jitihada na rasilimali hizo katika kufufua miradi iliyokufa na kuweka mfumo wa kufanya miradi iwe endelevu. Kwa hali ilivyo sasa, shabaha kubwa ya serikali imekuwa kujenga miradi mipya ya maji kuliko kuidumisha na kufufua miradi iliyopo.
 Mfano mdogo ni Kijiji cha Kipaduka, kilichopo kata ya Uhambingeto wilaya ya Kilolo ambapo kijiji hiki ni mojawapo ya vijiji kumi vitakavyopata mradi wa benki ya dunia. Kipaduka wamehamasishwa na wameunda kamati ya maji na kuchangisha shilingi milioni sita ambazo zipo benki zaidi ya miaka miwili sasa. Lakini kijiji kina vituo 10, nane havifanyi kazi na kamati haioni kuwa wanawajibika kutengeneza hivi vituo vilivyoharibika kwa vile wao wameandaliwa kwa ajili ya kusimamia mradi mpya.
 Hii inaonesha jinsi gani tupo tayari kujenga miradi mipya kuliko kuendeleza tuliyonayo.
Changamoto nyingine ya kuzingatia ni aina ya teknolojia tunayotumia na vipuli vyake. Jamii zimekuwa zikilalamika kuwa mashine na vifaa mbalimbali vya maji vimekuwa vikifa mara kwa mara.
Hali hii sio tu kwenye sekta ya maji, bali tumekuwa tukishuhudia bidhaa nyingi feki zikiingizwa hapa nchini. Hii inapelekea kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa miundombinu ya maji na kuwafanya wanajamii kushindwa kumudu. Hivyo serikali inapaswa kuchukua hatua ili kudhibiti haya.
Zipo sababu nyingi zaidi zinazosababisha miradi ya maji kufa mara kwa mara kama uelewa mdogo wa wanajamii katika kuiendesha miradi ya maji, halmashauri kukosa fedha za ufuatiliaji, na mengineyo. Cha msingi wadau wote tuibebe changamoto hii na kuifanyia kazi. Maadhimisho ya wiki ya maji yawe chachu katika kuleta kujadili changamoto hizi. Tukumbuke wananchi hawahitaji mipango, sera, magari, au hadithi nyingine zozote…wanahitaji maji.
Makala haya yamechapichwa kwenye Gazeti la Kwanza Jamii-IRINGA
Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa baruapepe richardlucas@daraja

HONGERA TBL KWA KUTAMBUA UMUHIMU WA MAJI KWA JAMII SI BIA TU

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (kushoto)  akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25, Mhandisi wa Maji  Wilaya ya Geita, Daud Sweka kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo za kusaidia mradi wa visima vitatu  vya maji safi na salama ya kunywa kwa wakazi wa Kijiji  cha Mkolani-1 wilayani humo hivi karibuni. Katikati ni Meneja Mauzo wa TBL Geita, Issa Msuya

SERIKALI NUSURU WANANCHI HAWA,TEMBO WACHACHAMAA-BUKOBA VIJIJINI



SERIKALI imeombwa kuweka mpango mkakati wa kupambana na wanyama waharibifu na kuwatoa katika mazingira wasipostairi ili kuepusha gharama nyingi za fidia zinazosababishwa na wanyama hao.

Rai imetolewa na baadhi ya wananch wa vijiji vya Ombweya na Kikagati vilivyoko katika kata ya Izimbya wilayani Bukoba vijijini,mara baada ya kufanya maojiano na waandishi wa habari waliofika maeneo hayo yanayodaiwa kukidhiri na kuwepo wanyama aina ya ya Tembo.

Bw.Januari Abdalla(35)mkulima wa maeneo hayo,alisema kuwa wanyama jamii ya Tembo ufanya uharibifu wa mazao ya wananchi kutokana na kutoka katika hifadhi ya Taifa Burigi iliyoko wilaya za Muleba na Buharamulo.

Abdalla alisema kuwa vitendo vya Tembo kuvamia makazi ya wananchi si jambo geni kwa wakazi hao,kwani ni kila mara wanyama hao ufanya uharibifu wa mali za watu na kuvunja vunja makazi yao,jambo ambalo ufanya wakazi husika kuishi kwa mashaka.

Bw. Bonifasi Rwegila ni meneja wa ranchi ya Taifa (NARCO)ya Kagoma iliyoko katika wilaya ya bukoba vijijini,alibainisha kuwepo na kushamili vitendo vinavyotokana na uvamizi wa wanyama hao.

Rwegila alisema kuwa wanyama hao ni hatari kwa maisha ya watu hususani watumishi ndani ya ranchi na wananchi jirani na ranchi hiyo,ambapo Tembo hao ufika mara kwa mara maeneo ya ranchi na kuharibu mazizi ya ng'ombe na majumba ya watumishi wa ranchi.

Alisema kuwa hali hiyo usababisha watumishi katika ranchi hiyo kuishi kwa tahadhari kubwa kwani mbali na kuvunja mazizi ya mifugo,Tembo pia ni hatari kwa maisha ya watu.

Meneja huyo wa Kagoma ranchi,alisema ni vyema serikali kupitia halmashauri za wilaya kuweka mpango maalumu ambao ni kwa ajili ya kufukuza wanyama hao mbali na maeneo ya watu kuliko kuendelea kufanya uharibifu ambao gharama uwa kubwa sana.

Alisema kuwa gharama za uendeshaji shughuli za ranchi ni kubwa mno,ikizingatiwa baadhi ya vitu kupandaa kwa bei madukani hivyo ni hasara kubwa pale inapotokea Tembo kuvunja mazizi ya mifugo wakati hali ya kiuchumi ni duni ambavyo wakati mwingine usababisha hata shughuli za uendeshaji kukwama.

Hata hivyo,pamoja na kusababisha gharama za uendeshaji wa ranchi kuwa kubwa,Meneja huyu alisema hali ya wasiwasi juu ya maisha yao kutokana na kuwepo na Tembo katika mazingira hayto,pia usabnabisha kufanya shughuli za kuvuga kwa roho mkononi,na kusababisha kuzorotesha ufanisi wa malengo yaliyokusudiwa.

Kero ya Tembo imekuwa ikilipotiwa mara kwa mara kwa wananchi wanaoishi maeneo ya kata za Izimbya na Kibirizi ingawa halmashauri ya wilaya Bukoba kupitia kitengo cha mali asili na Uvuvi, imekuwa ifanya utaratibu wa kuwafukuza wanyama hao na kuwasogeza mbali na maeneo wanamoishi wananchi,japo tatizo hilo linadaiwa bado kuwa ni kero kwa wananchi kwani kunauharifu mkubwa unaosabishwa na Tembo hao.

Tuesday, March 20, 2012

MCHUNGAJI ANYANGANYWA WATOTO KISA ADAIWA KUWANYANYASA!

Na.Kibuka Prudence,Bukoba Vijijini
HALMASHAURI ya wilaya Bukoba mkoani Kagera,imefikia uamuzi wa kutoa watoto waliokuwa wakipata malezi kutoka kwa mchungaji kutokana na kudaiwa kukiukwa na baadhi ya mashariti ya malezi.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na halmashauri Machi 17 chini ya idara ya maendeleo ya jamii,imekuja baada ya madai kuwa mlezi aliyekuwa akiwajibika kuwalea watoto hao 37 wakiwa wa kike 12 na kiume 25 alishindwa kufuata baadhi ya masharti yanayopaswa kufuatwa wakati wa malezi ya mtoto.

Mmoja wa maafisa wa idara hiyo waliohusika katika kuamisha watoto hao kutoka kituo cha malezi cha Kaagya Ophans Care Center na kuwaamisha kituo cha Kabilizi kilicho chini ya idara hiyo kata Rubale,bi.Renatha Mshwaili,alisema halmashauri imefikia maamuzi hayo ili kuepusha mtoto na matatizo mengine yanayoweza kumsababishia madhara ya kiafya.

Mshwaili alisema kuwa awali walibaini kuwepo matatizo mbalimbali yaliyokuwa baiona ya  mlezi wa kituo hicho ambaye ni mchungaji wa kanisa la Christian Life Church Cleoper Kaijage na mfadhili wa kituo hicho ambao ni shirika la The Mighty Fortress lenye makazi yake nchini Uholanzi.

Alisema baada ya mfadhili kudai kuwa hakubaliana na utawala uliopo na kuomba halmashauri kuchukua maamuzi juu ya walengwa(watoto)idara yake ilifikia maamuzi ya kuwanusuru watoto kwa mpango maalumu wa kujali usalama wa mtoto huku atua nyingine zikifuatwa.

Hata hivyo,kwa upande wake mlezi wa kituo hicho,mchungaji Kaijage,alikiri kutokubaliana na mfadhili wake kwa kile alichodai kuwepo baadhi ya wajumbe waliwai kufukuzwa ndani ya bodi ya kituo kumchonganisha mfadhili dhidi yake kwa maslahi ya kutaka utawala.

Mchungaji Kaijage aliswema kuwa japo kituo hicho kilikuwa kikipata ufadhili kutoka kwa shirika husika,lakini ufadhili ulimkuta tayari ameanza kutoa msaada kwa walengwa hao.Ambapo wazo la kuanzishwa kituo hicho lilianza tangu mwaka 2004 na mwaka 2005 alianza kutoa msaada wa malezi kwa watoto 12.

Alisema malezi hayo yaliendelea kutolewa kituoni hapo mpaka 2008 hini ya bodi ya kituo hicho,na tayari alikuwa amejenga majumba mawili japo yalikuwa ya udongo lakini lengo kuu lilikuwa ni kuwanusuru watoto wanaoishi katika mazingira magumu,ambao walickuliwa kutoka maeneo ya mwalo wa Igabilo na sehenmu nyingine.

Alisema msaada wa shirika ulianza kutolewa mnamo mwaka 2008 wakiwa na watoto 15,ambapo mfadhili alikubali kuwafadhili watoto kwa kuboresha nyumba na kutoa dola 20 kwa ajili ya chakula na matumizi mengine,jambo ambalo uongozi uliamua kulima ili kujipatia chakula na fedha hizo zikagharamikie huduma za kuwapatia elimu katika mashule mbalimbali.

Aidha,mchungaji huyo anadai kuwa anashangazwa na uamuzi wa halmashauri kumwamulisha ahame kituoni hapo kwa kuelekezwa na wafadhili,kwani yeye aende wapi wakati hapio alipo ndiyo kwake na kuiomba serikali kuchunguza kwanza na kubaini ukweli ulivyo kabla ya maamuzi mengine.

Alibainisha kuwa tayari ameanza kuchafuliwa kwa maneno ya kashifa kuwa anawanyanyasa watoto jambo ambalo ni la kupandikizwa na alishakamatwa na kukaa rumande kwa siku 15,japo tayari kesi dhidi ya madai yote yanayo muguza ipo mahakamani.

MWISHO

JAMANI HABARI ZINATAFUTWA BWANA SI KUKAA MJINI.....HAPA NI ZIZI LA NG'OMBE,MBOLEA YA KUTOSHA,WAKULIMA MKO WAPI?

Mojawapo ya mazizi makubwa katika ranchi za Taifa(NARCO)hii ni fursa kwa wakulima mkoani Kagera kufuata mbolea ya samadi katika maeneo ya ranchi za Taifa.

MOJAWAPO YA MAJOSHO YA KUOGESHA NG'OMBE KATIKA RANCHI YA KAGOMA

Ili ng'ombe waweze kunawili vizuri na kukabiliana na magonjwa mbalimbali ni vyema kuoshwa,anaeleza meneja ranchi ya Kagoma iliyopo wilaya ya Bukoba bw.Bonifas.

MIFUGO INAPATIKANA KAGOMA RANCHI.

Ng'ombe wanaopatikana katika ranchi za Taifa,Kagoma,Kikulula na Missenyi,pia jamii ya wafugaji wa Kagera unufaika kwa kupata mbegu bora za kufuga.

NG'OMBE JAMII YA KONGWA BEEF AINA HII YA MIFUGO INAPATIKANA RANCHI ZA TAIFA(NARCO)KAGOMA NA MISSENYI MKOANI KAGERA.

Na.Kibuka Prudence,Kagera
JAMII ya wafugaji wadogowadogo mkoani Kagera,wamepongeza uhamuzi wa mamlaka ya ranchi za taifa zinazojishughulisha na ufugaji wa ng'ombe,kwa kuwanufaisha kwa njia ya kutoa elimu ya ufugaji ulio bora ba wa kisasa.

Wakiongea na waandishi wa habari,wafugaji hao walisema utaratibu unaoendelezwa na kampuni za ranchi za Taifa(NARCO)zilizo Kagoma,Kikurula,Missenyi na Mabare ni mzuri na wenye malengo ya kumuinua mfugaji na mkulima ili kuondokana na umasikini.

Mmoja wa wafugaji hao John Muganyizi(47)mkazi wa wilayani Karagwe,alisema kuwa pamoja na baadhi ya wafugani wengine katika maeneo mbalimbali mkoani Kagera walikuwa na ujuzi wa kujiendeleza kiufugaji lakini utaratibu wa ranchi hizi ni mzuri zaidi kwani ni njia mbadala ya kumuelimisha mwananchi atambue umuhimu wa ufugaji na kilimo.

Muganyizi alisema kuwa awali hali ya ufugaji kwa wakulima ilionekana kukumbwa na changamoto kubwa ususani namna mbalimbali za kukabiliana na magonjwa ya mifugo,kubaini mbegu bora za ng'ombe zinazofaa katika ufugaji,lakini atua za ranchiNARCO kupisha utaratibu huu,ni dalili kuu inayoonesha kuwa serikali bado haijamsahau mfugaji wa taifa hili.

Alisema kwakuwa NARCO imeamua kuwapatia mafunzo wafugaji,ni vyema wakazi wa mkoa wa Kagera kuchangamkia fursa hii kwani ni muhimu na kwa kuelimika juu ya ufugaji janga la umasiki litapungua kwa kiasi kikubwa sana.

Tarsis Mawala ni meneja wa ranchi ya Missenyi,anasema utaratibu wa kutoa elimu ya ufugaji kwa wafugaji ni mojawapo ya majukumu ya NARCO hivyo ni mwendelezo wa mipango ya kampuni na ipo kwa kila mpango mkakati wa ranchi mkoani Kagera.

Mawala amesema pamoja na kutoa elimu pia ranchi hizo za Kagoma,Missenyi na Kikurula utoa mbolea kwa wakulima wa vijijini kwa bei nafuu sana,na kwa kufanya hivyo urahisisha ushughuli za ranchi na kujenga mahusiano kwa wananchi.

Alingeza kuwa hata hivyo kamppuni hizo ukabiliwa na baadhi ya changamoto nyingi mmojwapo ikiwepo uchomaji mbuga hovyo na kuwepo wanyama wakali maeneo ya ranchi kama tembo katika ranchi za Kagoma na Kikurula ambavo uhataarisha maisha ya watumishi wa ranchi na mifugo.

MWISHO


Friday, March 2, 2012

GENESTER MHAGAMA... HAKUELEWEKA......


Na.Kibuka Prudence,Bukoba
USHAURI juu ya viongozi wa Chama cha  Mapinduzi mkoani Kagera, kuhakikisha wanarudisha heshima ya chama hicho kwa wananchi kama ilivyokuwa hapo enzi za TANU,bado unasuasua kutekelezwa kwa baadhi ya makada wa chama hicho hapa nchini.

Bi.Genester Mhagama(mb)ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM,alitoa rai hiyo wakati wa sherehe za kuhadhimisha siku kuu ya saba saba ambayo ni maadhimisho ya kuzaliwa TANU zilizofanyika ndani ya manispaa ya Bukoba mkoani Kagera,mwaka jana.

Mhagama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,alikaririwa kuwa chama cha mapinduzi kimekuwa na changamoto nyingi hasa baada ya miaka ya hivi karibuni kutokana na ndani ya cha hicho kuwemo baadhi ya watu wengine wenye dhamira tofauti na ile iliyodhamiliwa na hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Mtazamo huo  kwa wanaCCM,kwa kuwataka kubadilika kifikra na kivitendo ili jamii iweze kunufaika na miaka 50 ya Uhuru, na kusisitiza kuwa viongozi pamoja na wapenzi na wakereketwa wa CCM hawana budi kuanza kurudisha imani ya chama  kwa wananchi wote wa Tanzania kwa kufuata misingi na kuheshimu miiko aliyoiacha muasisi wa taifa hili
.
Hata hivyo,ingawa kada huyo alitoa elimu hiyo kwa  wana CCM,inawezekana baadhi yao hawakuelewa kile alichosema Mhagama,kwani hali ya mvutano kwa baadhi ya wanaCCM hasa Bukoba vijijni,inaendelea kuwa na mashakani na kuleta wasiwasi kwa jamii. 

Hasa kuendelea kuwepo makundi tofauti huku mengine yaskionekana kusononeshwa na matokeo ya uchaguzi mkuu uliomalizika 2010,jambo ambalo linachangia kuanza kuibuka kwa vikundi mbalimbali ambavyo vinaanza kuandaa wagombea wa majimbo ya ubunge kwa kuwatembeza baadhi ya watarajiwa wa nafasi hizo.

Hali hiyo inaonekana kuwa ‘tete’na kushamiri katika jimbo la Bukoba vjijini ambapo baadhi ya wagombea walioshindwa katika kinyanganyiro hicho katika kura za maoni,tayari wameanza kupitisha nyaraka zilizochapishwa juu ya ahadi zilizoahidiwa na mbunge wa sasa Jasson Rweikiza na kuwaonyesha wananchi kwa madai kashindwa kuzitimiza.
MWISHO

TUHESHIMU NA KUENZI ZANA ZA MABABU ZETU

Mmojawapo ya kazi zinazofanywa na kikundi cha BUDAP kinachounganisha baadhi ya wenye ulemavu mjini Bukoba...........karibu uoneeeeeeee!

UBUNIFU NI MTAJI NDUGU YANGU.

 Mmoja wa wenye ulemavu akitoa maelezo kwa mwenzake juu ya ufundi katika kutengeneza ngoma na vitu mbalimbali kwa kutumia ngozi ya ng'ombe.Utaalamu huu utaupata mjini Bukoba.

LOOH!.... MNAKUMBUKA TULIKOTOKA....?

UTAMADUNI ni muhimu sana,hii ni nyumba ya Msonge maarufu kwa jina la 'Nyaruju'ni ukumbusho wa utamaduni wa MHAYA.

BWAWA LA KUFUGIA SAMAKI WILAYANI MULEBA

 Hili ni bwawa la kufugia samaki  lililopo kata Muhutwe mkoani Kagera







Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Henry Salewi akizungumza na waandishi wa habali juu ya usalama wa raia na mali zao mjini Bukoba

 UTALII TUNAJIFUNZA SISI WANA HABARI WA KAGERA
Meneja wa kampuni ya utalii ya Kiroyela Tours ya mjni Bukoba mwenye suti nyeusi akiwapa maelekezo waandishi wa habari wa mkoani Kagera juu ya huduma zinazotolewa na kampuni hiyo