KYAKA-MISSENYI
UONGOZI wa kiwanda cha sukari cha Kagera(Kagera Sugar Limited)uesema kuwa bei
ya sukario haipandishwi kiholela kwa maslahi ya kiwanda bali ni kutokana
na kuwepo gharama kubwa za uzalishaji kiwandani.
Akiongea na
mwandishi wa habari hizi,mmoja wa watendaji wakuu katika kiwanda
hicho,Vicent Mtaki,amekiri kuwa ni kweli bei ya sukari kwa wananchi wa
mkoa wa Kagera ni ya juu kulinganisha na miaka ya nyuma lakini lazima na
jamii itambue kuwa kiwanda kinatumia gharama kubwa hadi kufikia atua ya
kuzalisha sukari.
Mtaki alisema kuwa kuwepo na gharama kubwa
kunatokana na mkoa wa Kagera kuwa mbali sana na jiji la Dar es salaamu
ambapo,mahitaji mengi juu ya shughuli za uzalishaji yanapatikana huko.
Alisema
kuwa mkoa wa Kagera huko pembezoni mwa nchi,tofauti na mikoa mingine
yenye viwanda vya kuzalisha sukari kama
Morogoro ambapo ni rahisi kuchukua malighafi(raw materials)jijini Dar
es salaamu tofauti na Kagera ambako ni vigumu kuzalisha sukari na kuiuza
kwa bei ya chini huku kila mahitaji ya uzalishaji yanategemewa
kupatikana Dar es salaam.
"Kuanzia chuma,mafuta ya Disel,pembejeo
za kilimo,madawa nk vyote tunavinunua Dar es salaam,gharama inakuwa juu
hasa kwa kipindi hiki cha mtikisiko wa uchumi duniani,hivyo tunalazimu
kuzalisha kiwango ambacho tunakisambaza mikoa hasa ya Kagera na Mwanza
ili kuepuka hasara kubwa kwani mbali na maeneo hayo kiwanda kitaingia
hasara kubwa sana"alisema Mtaki.
Alisha kutokana na changamoto
hiyo,inakuwa vigumu kiwanda kusambaza sukari kwa mikoa mingine tofauti
na tajwa kwani iwapo kiwanda kitalazika kufanya hivyo,lazima bei ipande
zaidi kwa wakazi wa mikoa mingine kutokana kuwepo na gharama za
usafirishaji.
Hata hivyo,Mtaki amewatoa wasiwasi wananchi wa Kagera kuwa bei ya sukari kamwe haiwezi kuendelea kubaki
pale ilipo,kwani watarajie kushuka iwapo hali ya mfumuko wa bei utakapo kuwa umepungua.
Kauli
hiyo kwa uongozi wa kiwanda imekuja mara baada ya kuwepo minongono
mingi kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kuhusu kutoshuka bei ya sukari
ambapo hadi sasa kilo moja ya sukari inanunuliwa kati ya bei ya shilingi
2000/= hadi 2500/=jambo ambalo linawakatisha tamaa ya maisha wananchi
huku wengi wakilinganisha iweje bei ya cement iuzwe 20000 kwa mfuko na
ikiwa jijini Dar es Salaam iuzwe kati ya 13500 au 14000/=.
No comments:
Post a Comment