Bukoba Vijijini-KAGERA
WAKULIMA mkoani Kagera
wameshauliwa kutumia mbolea aina ya samadi inayopatikana kwa wingi
katika sehemu za ranchi za Taifa(NARCO)ili kukabiliana na changamoto za
udongo kukosa rutuba kwa baadhi ya maeneo mbalimbali ya kilimo cha mazao
mbalimbali.
Akiongelea juu ya matumizi ya samadi, meneja wa ranchi ya Taifa(NARCO)
ya Kagoma,Boniphasi Rwegila,alisema kuwa ni fursa pekee kwa wakazi wa
mkoa wa Kagera kutumia ranchi zilizomo mkoani hapa kwa matumizi ya
kilimo cha kisasa,jambo ambalo litawasaidia kupambana na umasikini wa
kipato.
Rwegila alisema kuwa mbolea nyingi aina ya samadi iliyopo
ndani ya ranchi ni mmojawapo ya fursa tosha wanayopata kunufaika nayo
wananchi kwa kulipia gharama nafuu na kuchukua mbolea kwa madhumuni ya
kulima na kuotesha mazao mengi.
Alisema kuwa ranchi(NARCO)imekuwa
na utaratibu wa kutoa
elimu kwa wananchi juu ya manufaa yanaoweza kupatika kwa kutumia ranchi
za taifa,ikiwemi kuhamasisha wananchi kufika maeneo ya ranchi na
kuchukua mbolea kwa kulipia gharama kidogo,lengo ni kuwawezesha wananchi
ili kunufaisha na rasilimali zao za Taifa.
Pia,alibainisha kuwa
maeneo mengi mkoani Kagera yamekuwa yakitajwa kukosekana na rutuba na
wakati mwingine huwa vigumu hata utumiaji wa mbolea za viwandani kwani
pamoja na kuwa na gharama kubwa pia mila uchangia wananchi
kutoshawishika kuzitumia mbolea hizo.Hivyo ni bora jamii ikahamasika
kutumia mbolea(Samadi)inayopatikana kwa urahisi na inayokubarika kwa
udongo wa mazingira husika.
Mbali na upatikanaji wa mbolea aina
ya samadi kwa wingi,katika ranchi ya Taifa ya Kagoma iliyoko wilaya ya
Bukoba vijijini na kupakana na wilaya za Muleba na Karagwe,pia ranchi
hiyo inazalisha mbegu bora za ng'ombe ijulikanayo kwa jina
'Morani'ambazo usambazwa kwa wafugaji wadogo wadogo vijijini.
Rwegila
alisema kuwa mpango wa kuzalisha mbegu bora aina ya Morani,umefanikiwa
kwa kiasi kikubwa lengo la NARCO ni kuzalisha mbegu bora ya ng'ombe
ambayo ina sifa ya kukua haraka,kuwa na nyama nzuri na kutoa maziwa
mengi,hivyo ni muhimu kwa mkulima mdogo wa kijijini kwa kufuga mbegu
inayo kua haraka na yenye soko kwa mahitaji ya sasa na kesho.
"Tumefanikiwa
kwa kutoa mbegu bora za Morani na tumezisambaza kwa wakulima
vijijini,ili waweze kubadirisha mbegu yao ya zamamani ijukana kwa jina
la 'Nkole'ambayo uchelewa kukua na haitoi maziwa mengi kwa
mfugaji"alisema Rwegila.
Hata hivyo,pamoja na malengo hayo juu ya
kuinua pato la mkulima,pia zilitajwa baadhi za changamoto zinazokabili
ranchi ya (NARCO)Kagoma,ikiwani mifugo kushambuliwa magonjwa ambayo
yanadaiwa kutokana na baadhi ya mifugo kutoka kwa majirani wa ranchi na
kusababisha shughuli za uendeshaji kuwa ngumu.
Alisema kuwa
changamoto ya magonjwa ni chanjo ambapo madawa ni ghali mno na hii
ni kutokana na serikali kujitoa kuhudumia ranchi za Taifa(NARCO)hivyo
na kufanya ranchi zenyewe kujitegea katika shughuli za uendeshaji bila
ruzuku ya uendeshaji kutoka serikali.
Kampuni ya ranchi za
Taifa(NARCO)inamiliki ranchi nne mkoani Kagera ambazo ni Kagoma iliyoko
wilaya ya Bukoba vijijini,Missenyi na Mabale zikiwa wilayani Missenyi
huku Kikurula ikiwa wilayani Karagwe.
No comments:
Post a Comment