Na.Kibuka Prudence,Bukoba Vijijini
HALMASHAURI ya wilaya Bukoba
mkoani Kagera,imefikia uamuzi wa kutoa watoto waliokuwa wakipata malezi
kutoka kwa mchungaji kutokana na kudaiwa kukiukwa na baadhi ya
mashariti ya malezi.
Hatua hiyo iliyochukuliwa na halmashauri Machi 17 chini ya idara ya maendeleo ya jamii,imekuja baada ya madai kuwa
mlezi aliyekuwa akiwajibika kuwalea watoto hao 37 wakiwa wa kike 12 na
kiume 25 alishindwa kufuata baadhi ya masharti yanayopaswa kufuatwa
wakati wa malezi ya mtoto.
Mmoja wa maafisa wa idara hiyo
waliohusika katika kuamisha watoto hao kutoka kituo cha malezi cha
Kaagya Ophans Care Center na kuwaamisha kituo cha Kabilizi kilicho
chini ya idara hiyo kata Rubale,bi.Renatha Mshwaili,alisema halmashauri
imefikia maamuzi hayo ili kuepusha mtoto na matatizo mengine yanayoweza
kumsababishia madhara ya kiafya.
Mshwaili alisema kuwa awali walibaini kuwepo matatizo
mbalimbali yaliyokuwa baiona ya mlezi wa kituo hicho ambaye ni
mchungaji wa kanisa la Christian Life Church Cleoper Kaijage na
mfadhili wa kituo hicho ambao ni shirika la The Mighty Fortress lenye
makazi yake nchini Uholanzi.
Alisema baada ya mfadhili kudai
kuwa hakubaliana na utawala uliopo na kuomba halmashauri kuchukua
maamuzi juu ya walengwa(watoto)idara yake ilifikia maamuzi ya
kuwanusuru watoto kwa mpango maalumu wa kujali usalama wa mtoto huku
atua nyingine zikifuatwa.
Hata hivyo,kwa upande wake mlezi wa
kituo hicho,mchungaji Kaijage,alikiri kutokubaliana na mfadhili wake
kwa kile alichodai kuwepo baadhi ya wajumbe waliwai kufukuzwa ndani ya
bodi ya kituo kumchonganisha mfadhili dhidi yake kwa maslahi ya kutaka
utawala.
Mchungaji Kaijage aliswema kuwa japo kituo hicho
kilikuwa kikipata ufadhili kutoka kwa shirika husika,lakini ufadhili
ulimkuta tayari ameanza kutoa msaada kwa walengwa hao.Ambapo wazo la
kuanzishwa kituo hicho lilianza tangu mwaka 2004 na mwaka 2005 alianza
kutoa msaada wa malezi kwa watoto 12.
Alisema
malezi hayo yaliendelea kutolewa kituoni hapo mpaka 2008 hini ya bodi
ya kituo hicho,na tayari alikuwa amejenga majumba mawili japo yalikuwa
ya udongo lakini lengo kuu lilikuwa ni kuwanusuru watoto wanaoishi
katika mazingira magumu,ambao walickuliwa kutoka maeneo ya mwalo wa
Igabilo na sehenmu nyingine.
Alisema msaada wa shirika ulianza
kutolewa mnamo mwaka 2008 wakiwa na watoto 15,ambapo mfadhili alikubali
kuwafadhili watoto kwa kuboresha nyumba na kutoa dola 20 kwa ajili ya
chakula na matumizi mengine,jambo ambalo uongozi uliamua kulima ili
kujipatia chakula na fedha hizo zikagharamikie huduma za kuwapatia
elimu katika mashule mbalimbali.
Aidha,mchungaji huyo anadai
kuwa anashangazwa na uamuzi wa halmashauri kumwamulisha ahame kituoni
hapo kwa kuelekezwa na wafadhili,kwani yeye aende wapi wakati hapio
alipo ndiyo kwake na kuiomba serikali kuchunguza kwanza na kubaini
ukweli ulivyo kabla ya maamuzi mengine.
Alibainisha
kuwa tayari ameanza kuchafuliwa kwa maneno ya kashifa kuwa
anawanyanyasa watoto jambo ambalo ni la kupandikizwa na alishakamatwa
na kukaa rumande kwa siku 15,japo tayari kesi dhidi ya madai yote
yanayo muguza ipo mahakamani.
MWISHO
No comments:
Post a Comment