Na.Kibuka Prudence,Bukoba
USHAURI juu ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi
mkoani Kagera, kuhakikisha wanarudisha heshima ya chama hicho kwa wananchi kama
ilivyokuwa hapo enzi za TANU,bado unasuasua kutekelezwa kwa baadhi ya makada wa
chama hicho hapa nchini.
Bi.Genester Mhagama(mb)ambaye pia ni mjumbe wa
kamati kuu ya CCM,alitoa rai hiyo wakati wa sherehe za kuhadhimisha siku kuu ya
saba saba ambayo ni maadhimisho ya kuzaliwa TANU zilizofanyika ndani ya manispaa
ya Bukoba mkoani Kagera,mwaka jana.
Mhagama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la 10
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,alikaririwa kuwa chama cha mapinduzi
kimekuwa na changamoto nyingi hasa baada ya miaka ya hivi karibuni kutokana na
ndani ya cha hicho kuwemo baadhi ya watu wengine wenye dhamira tofauti na ile
iliyodhamiliwa na hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Mtazamo huo kwa wanaCCM,kwa kuwataka kubadilika kifikra na
kivitendo ili jamii iweze kunufaika na miaka 50 ya Uhuru, na kusisitiza kuwa viongozi
pamoja na wapenzi na wakereketwa wa CCM hawana budi kuanza kurudisha imani ya
chama kwa wananchi wote wa Tanzania kwa
kufuata misingi na kuheshimu miiko aliyoiacha muasisi wa taifa hili
.
Hata hivyo,ingawa kada huyo alitoa elimu hiyo
kwa wana CCM,inawezekana baadhi yao
hawakuelewa kile alichosema Mhagama,kwani hali ya mvutano kwa baadhi ya wanaCCM
hasa Bukoba vijijni,inaendelea kuwa na mashakani na kuleta wasiwasi kwa jamii.
Hasa kuendelea kuwepo makundi tofauti huku
mengine yaskionekana kusononeshwa na matokeo ya uchaguzi mkuu uliomalizika
2010,jambo ambalo linachangia kuanza kuibuka kwa vikundi mbalimbali ambavyo
vinaanza kuandaa wagombea wa majimbo ya ubunge kwa kuwatembeza baadhi ya
watarajiwa wa nafasi hizo.
Hali hiyo inaonekana kuwa ‘tete’na kushamiri
katika jimbo la Bukoba vjijini ambapo baadhi ya wagombea walioshindwa katika
kinyanganyiro hicho katika kura za maoni,tayari wameanza kupitisha nyaraka
zilizochapishwa juu ya ahadi zilizoahidiwa na mbunge wa sasa Jasson Rweikiza na
kuwaonyesha wananchi kwa madai kashindwa kuzitimiza.
MWISHO
No comments:
Post a Comment