KEMONDO -BUKOBA.
WAFANYAKAZI wa kiwanda cha kusindika minofu ya samaki cha
Kagera Fish Company ltd kilicho katika kata ya Kemondo wilayani
Bukoba,wameulalamikia uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwafanyia vitendo vya
uzalilishaji na kubambikiziwa kesi pale wanapodai haki zao za malipo.
Wafanyakazi hao(30) ambao majina yao yameifadhiwa kwa
usalama wao,wamesema mwajili wao ambaye yamemtaja kwa jina moja la Awadesh
ambaye ana asili ya kieshia kuwa amekuwa akiwatukana matusi ya uzalilishaji na
kuwatishia kufunga iwapo wakiendelea kudai madai yao pale wanapokuwa wakidai
haki zao kutokana na kazi wanazofanya kiwandani hapo.
Wameeleza kulazimishwa kufanya kazi nyingi kwa muda mwingi
kuanzia asubuhi hadi asubuhi ya siku nyingine bila kupewa malipo ya ziada(over
time)na wanapodai malipo yao,mwajili(Awadesh)umpigia simu mkuu wa kituo cha
Polisi Kemondo(OCS)ambaye ufika mara moja na kuwakamata na kuwaweka maabusu.
Wamebainisha mhindi huyo(Awadesh)utumia muda mwingi kwa
kuwatusi kwa kuwaita ‘nyani’jambo ambalo linawadharirisha na linaonyesha wazi
kuwa hawadhaminiki kama binadamu mbele ya mwajili wao huyo japo kazi
wanazozifanya ni nyingi na zinaingia uchumi taifa.
Aidha,wamesema kuwa mbali na kufanyakazi katika mazingira
magumu,matusi yanazidi kila siku wawapo kazini huku wakimtaja Dayari Sin ambaye
pia ni meneja uzalishaji(Production Manager) kiwandani hapo kuwa uwatusi na
kuwakejeli kuwa hata waende kushitaki wapi hakuna watakaposikilizwa kwani
hawana fedha.
“Ni muda mrefu tumedhurumiwa haki zetu,tukidai haki zetu
tunakamatwa na polisi na kulazwa ndani,tunabambikiziwa kesi zisizo za
kweli.huku wenzetu hawa(wahindi)wanatudharirisha na kusema wazi kuwa Serikali yetu haina akiri,askari kuja
chukua fedha kiwandani na kuondoka”walisema wahanga wa manyanyaso hayo.
Wamesema kuwa wanashangazwa kuona wahindi wanatumia kituo
cha serikali yetu chenye dhamana ya kulinda usalama wetu,kutukandamiza na
kudhurumu haki zetu kama vile kipo kwa ajili ya wamiliki wa kiwanda tu.
Alipotafutwa meneja mkuu wa Kiwanda hicho Awadesh hakutaka
kuongelea juu ya jambo hilo mpaka alipomruhusu afisa utumishi wake Wilson John
kuwa ndiye wakuongelea suala hilo.
Hata hivyo Wilson alikiri kuwepo hali hiyo ndani ya kiwanda
hicho,na kudai kuwa yeye haoni sababu ya wafanyakazi kuendelea kuvurugana na
mwajili wao,kama walikuja kufanya kazi ni bora wakubaliane na matakwa ya
mwajili iwapo hawako tayari bora waache waende kwingine.
Alipoulizwa kuhusu kuwepo matunizi ya kituo cha polisi kwa
maslahi ya kiwanda na nia ya kuwakandamiza wafanyakazi,alijibu kuwa hiyo hipo
juu ya uwezo wake kwani ni mahusiano yaliopo baina ya mkuu wa kituo na kiwanda
hicho.
Aidha,baadhi ya wakazi wa Kemondo wamelaani askari kutumiwa
na kiwanda kuwakamata watendaji kwa kuwabambikizia kesi zisizo za kweli,kwani
zipo nia za askari kufanya uchunguzi kabla ya kuingilia masuala ya watumishi
hao.
Walisema kuwa mbali na madai hayo,kiwanda hicho pia
kinakasoro kibao zikiwemo za kikwepa ushuru wa kulipia mabondo,kuwa na njama za
kuyasafirisha usiku kwenda nchini Uganda.Na kuingiza samaki walio chini ya
kiwango kinachokubalika(undersize)hasa wakati wa usiku wakidai serikali usiku
uwa imelala.
Kiwanda cha kusindika minofu ya samaki cha Kagera Fish
Company ltd,kina ubia na mwekezaji wa ndani Nadhir Karamagi kwa kushirikiana na
menegimenti ya kiwanda kingine cha kusindika minofu cha Omega kilicho jijini
Mwanza,kina jumla ya wafanyakazi wa kudumu 30 pamoja na vibarua zaidi ya 70.
No comments:
Post a Comment